Psalms 46

Mungu Yuko Pamoja Nasi

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi.

1 aMungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 bKwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa
nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.
3 cHata kama maji yake yatanguruma na kuumuka,
milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.

4 dKuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu,
mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.
5 eMungu yuko katikati yake, hautaanguka,
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6 fMataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka,
Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka.

7 g Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

8 hNjooni mkaone kazi za Bwana
jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9 iAnakomesha vita hata miisho ya dunia,
anakata upinde na kuvunjavunja mkuki,
anateketeza ngao kwa moto.
10 j“Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu;
nitatukuzwa katikati ya mataifa,
nitatukuzwa katika dunia.”

11 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi;
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Copyright information for SwhNEN